Katika ulimwengu wa sasa, huwa ni kama hitaji la msingi kijana kuwa na ujuzi wa kutumia kompyuta.
Ni ujuzi unaohitajika katika maeneo mengi ya kazi na hata katika kutekeleza shughuli za kila siku.Lakini kwa vijana wengi ambao hukosa nafasi ya kujiunga na shule au vyuo vinavyotoa mafunzo ya kompyuta, huwa vigumu sana kupokea ujuzi huu.
Lakini wakfu wa shirika la Craft Silicon Foundation, unaomilikiwa na kampuni ya kuuza programu za kompyuta, umeanzisha mradi unaowawezesha vijana kujifunza kutumia komputa ndani ya basi ambalo ni darasa.
"Mimi natoka Kibera, kwa sababu nimejaribu kutafuta pesa ili niweze kujilipia masomo ya kompyuta. Kazi ninayoifanya mapato ni ya chini sana sijapata pesa ambazo zinaweza kunisaidia ili niweze kulipia masomo hayo," anasema mmoja wa wanafunzi hao, Wesley Soi.
"Masomo haya yamenisaidia sana."
Basi hilo huhudumia vijana maskini katika mitaa ya Kawangware, Mukuru, Korogocho, Kibera na Mathare.


Chapisha Maoni