Leo September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
jimbo la Temeke kimechukua headlines baada ya kufanya maamuzi ya
kumfukuza uanachama Diwani na Mwenyekiti wake kutoka kata ya Kurasini, Matiti Claudian Togocho kutokana na kashfa ya ufisadi wa zaidi ya shilingi milioni 400 alizozipata kwa njia ya udanganyifu.
Taarifa iliyotolewa na Benard Mwakyembe
ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke imeeleza kuwa mnamo
November 23 2015, Diwani huyo akiwa na wenzake wanadaiwa walitengeneza
hati feki ya nyumba tano za James Makundi aliyekuwa
mpangaji kwenye nyumba zake kisha kufanya hujuma ya kuvunja nyumba hizo
kwa amri ya uongo ilitolewa na wakili kishoka wa Samora Avenue badala ya
amri ya mahakama ikiwa ni kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa
mwekezaji ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.
Diwani huyu pia anahusishwa na matukio mengine mawili ya udhulumaji wa zaidi ya shilingi milioni 140 za mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni
wakati kesi ikiwa mahakamani pamoja na fedha za fidia za Paulina Shaban
na wajukuu zake ambao Diwani huyo alisimamia nyumba zao kubomolewa.

Chapisha Maoni