NI Sept 20, 2016 ambapo msanii kutoka
Bongo Movie, Dude amefunguka kuhusu maandalizi ya kuirudisha kipindi cha
Bongo Dar es Salaam katika luninga.
Akiongea na millardayo.com & Ayo TV staa huyo alisema…>>>Kwanza
nilikuwa najaribu kufanya mazungumzo na wamiliki wa vituo vya luninga
ili niweze kurusha kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam na sio kama
nahitaji pesa nyingi sana lakini nahitaji aghalau nirudishe maandalizi
ya kazi yangu’
‘Takribani
tukiacha mwezi huu wa tisa upite tutegemee mwezi wa kumi nadhani kila
kitu kitakuwa vizuri na nitaweza kutengeneza vipindi vingi zaidi na
mwezi wa kumi nina uhakika kabisa kuwa kipindi kitakuwa hewani lakini
sitotaka kuwaambia mashabiki zangu kuwa ni TV gani kitakuwa kinarusha
ila wakae mkao wa kula’

Chapisha Maoni